Monday, July 23, 2012

KUSUDI LA MUNGU KWA MWANADAMU

kila mwanadamu anamazingila aliyoumbiwa,ukisha kuja duniani unamiti miwil.

Mungu anapomleta mwanadamu duniani anakua ameshapanga kitu gani anaenda kufanya.
Uji duniani Mungu iliakutafutie kazi

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana,ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi siku zenu za mwisho. Ndo inavotwambia YER:29:11 

Ona Mungu anavotupenda, katika WAEFESO:1:4 Anazidi kusema, angalia..kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla yakuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.  zidi kuona anavotuangaikia....

2WAKORINTHO:2:11 Anasema Shetani asije akapata kutushinda, kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.

Ona sasa  hii 2WAKORINTHO 11:3 anasema lakini nachelea, kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu,mkauacha unyofu na usafi kwa kristo. kumbe Hawa ndo alidanganywa Adamu hakudanganywa.. ona sasa hii...1TIMOTHEO: 2:14 inasema...Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 

Sikia hii mtu wa Mungu.. kumbe masaa yote inabidi tukae tayari maana shetani yuko vitani mda wote na masaa yote WAEFESO: 6:11 inasema vaeni siraha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga ila za shetani.

Sunday, July 22, 2012

JE,WAJUA MAOMBI YA TOBA KATIKA MALANGO NA FAIDA ZAKE?

 Wapendwa, Bwana yesu asifiwe! Natumai wazima wa afya wote. katika neno letu la leo tungependa kujifunza namna ya Toba katika malango ilivo na faida kubwa kwetu..katika kitabu cha NEHEMIA.12:27-30 inasema, Basi walipouweka wakfu ukuta wa yerusalemu, wakawatafuta walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta yerusalemu,wapate kufanya wakfu pamoja na furaha,na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi. waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya yerusalemu na kutoka vijiji vya wanetofathi tena toka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi, kwa maana waimbaji hao walikua wamejijenga vijiji katika viunga vya Yerusarem. Makuhani na Walawi wakajitakasa nao wakawatakasa watu na malango na ukuta. UFUNUO WA YAHANA 21:1-3 Inatwambia kua, kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi yya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusaremu mpya ,ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu umewekwa tayari, kama bibi-harusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Yapo mengi yaliyoandikwa kuhusu Malango..tutazidi kuona namna toba ilivo na faida sana  juu ya malango.

Thursday, July 19, 2012

"MATUKIO KATIKA AJALI YA MV.SEAGUL"



                    mh.kikwete akiangalia maiti za watoto katika ajali iyo