Sunday, July 22, 2012
JE,WAJUA MAOMBI YA TOBA KATIKA MALANGO NA FAIDA ZAKE?
Wapendwa, Bwana yesu asifiwe! Natumai wazima wa afya wote. katika neno letu la leo tungependa kujifunza namna ya Toba katika malango ilivo na faida kubwa kwetu..katika kitabu cha NEHEMIA.12:27-30 inasema, Basi walipouweka wakfu ukuta wa yerusalemu, wakawatafuta walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta yerusalemu,wapate kufanya wakfu pamoja na furaha,na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi. waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya yerusalemu na kutoka vijiji vya wanetofathi tena toka Beth-gilgali, na toka mashamba ya Geba na Azmawethi, kwa maana waimbaji hao walikua wamejijenga vijiji katika viunga vya Yerusarem. Makuhani na Walawi wakajitakasa nao wakawatakasa watu na malango na ukuta. UFUNUO WA YAHANA 21:1-3 Inatwambia kua, kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa maana mbingu za kwanza na nchi yya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusaremu mpya ,ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu umewekwa tayari, kama bibi-harusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Yapo mengi yaliyoandikwa kuhusu Malango..tutazidi kuona namna toba ilivo na faida sana juu ya malango.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment