PRESS RELEASE:
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA, GOSPEL, DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa
ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel,
Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agizo kwenu la
kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na
Callertunes katika mitandao ya simu ya VodaCom, Zantel, Tigo na Airtel
na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako
mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa
muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya
sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu
ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya
biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka
wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika
kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu
ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni
asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili
linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya
pato toka kwenye shoo.
Hivyo
tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa
maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi
zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa
pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu
kwa njia ya Television, Radio, blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi
wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho
tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili
kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.
No comments:
Post a Comment